19 Kwa hekima Yawe aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu.
Ee Yawe, matendo yako ni mengi sana! Umeyafanya kwa hekima yote! Dunia imejaa viumbe vyako!
Yawe aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake alisimamisha ulimwengu imara, kwa akili yake alizitandika mbingu juu.
Vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, wala hakuna hata kitu kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
Yawe ndiye aliyeumba dunia kwa nguvu zake, aliyeuimarisha ulimwengu kwa hekima yake, na kwa akili yake akazitandaza mbingu.
Aliumba mbingu kwa hekima. Wema wake unadumu milele.
“Yawe aliniumba kwa mwanzo wa kazi yake, zamani za kale mbele ya kuumbwa kwa kitu chochote.
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Uniambie, kama una maarifa.