15 Hekima ni ya maana sana kuliko mawe ya bei kali, hakuna kitu unachotamani kinachoweza kulingana nayo.
“Hekima ina maana sana kuliko mawe ya bei kali; kitu chochote unachotamani hakiwezi kulingana nayo.
Hekima ina bei kali kuliko mawe ya matumbawe na marijani, bei kali yake inashinda bei kali ya ushanga.
Ninaona kwamba mateso ya wakati huu wa sasa hayawezi kupima kulinganishwa na utukufu ambao Mungu atakaoonyesha kwetu waziwazi.
Muke mwema atapatikana wapi? Bei yake ni kali kuliko ushanga!
Kuna zahabu na wingi wa mawe ya bei kali; lakini kitu cha bei kali zaidi ni maneno ya maarifa!
Nina hamu ya kukuona katika pahali pako patakatifu, nione nguvu yako na utukufu wako.
Chagua mafundisho yangu pahali pa feza; na maarifa pahali pa zahabu safi.
Hekima ni ya bei kubwa kama urizi; ni ya mafaa kwa wale wote wanaokuwa wazima.