Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Matayo 4:12 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

12 Yesu aliposikia kwamba Yoane ametiwa katika kifungo, akaenda zake Galilaya.

Gade chapit la Kopi




Matayo 4:12
13 Referans Kwoze  

Nyuma ya kutiwa kwa Yoane katika kifungo, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema inayotoka kwa Mungu.


Lakini Herode akaongeza ubaya mwingine kwa kumutia Yoane ndani ya kifungo.


Herode alikuwa amemukamata Yoane akamufunga minyororo na kumutia ndani ya kifungo. Herode alifanya vile kwa sababu ya Herodia, muke wa ndugu yake Filipo.


(Wakati ule Yoane alikuwa hajawekwa katika kifungo.)


Yesu akarudia Galilaya akijazwa na uwezo wa Roho, na habari zake zikaenea fasi zote katika pande zile.


Ni Herode mwenyewe aliyeamuru kwamba Yoane akamatwe na kutiwa katika kifungo. Ilitokea vile kwa sababu Herode alimwoa Herodia, muke wa ndugu yake Filipo.


Hiki ndicho kitambulisho cha pili Yesu alichoonyesha. Ilikuwa wakati aliporudi Galilaya akitoka Yudea.


Siku mbili zilipopita, Yesu akaondoka kule, akaenda Galilaya.


Halafu Yesu akaenda Kapernaumu, katika jimbo la Galilaya. Siku ya Sabato ilipotimia, akawafundisha watu.


Yoane Mubatizaji, akiwa katika kifungo, akapata habari za mambo Kristo aliyokuwa akifanya. Basi akawatuma wanafunzi wake


Lakini wakazidi kusema kwa nguvu: “Kwa njia ya mafundisho yake anawashawishi watu kufanya uasi katika Yudea yote. Alianzia Galilaya na sasa amefika hapa.”


Siku iliyofuata Yesu alitaka kwenda Galilaya. Alipomukuta Filipo akamwambia: “Unifuate.”


Ni vile Yesu alivyofanya kitambulisho chake cha kwanza katika Kana ya Galilaya. Pale alionyesha utukufu wake na wanafunzi wake wakamwamini.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite