Utakoleza sadaka zako zote za ngano kwa chumvi. Usiache hata kidogo kuweka chumvi katika sadaka yako ya ngano, maana chumvi ni kitambulisho cha agano Mungu alilofanya pamoja nanyi.
“Ninyi ni kama chumvi kwa watu wote. Lakini kama chumvi ikipoteza onjo lake, itatiwa nini ipate tena kukolea? Haifai tena hata kidogo, inabakilia kutupwa na kukanyagwa na watu.
“Chumvi ni kitu kizuri. Lakini chumvi ikipoteza onjo lake, itatiwa nini kusudi ipate tena kukolea? “Muwe na chumvi ndani yenu na muishi pamoja kwa amani.”