Siku ile ilikuwa ya matayarisho ya siku ya Sabato iliyofuata. Kwa sababu hii Wayuda hawakutaka maiti za wale waliotundikwa zibaki juu ya misalaba kwa maana siku ile ilikuwa kubwa sana. Kwa hiyo wakamwomba Pilato ruhusa kwamba miguu ya wale waliotundikwa ivunjwe kusudi wakufe mbio na maiti zao ziondoshwe.