Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.
Na yote yaliyoandikwa zamani katika Maandiko Matakatifu yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi, kusudi tuendelee kuchunga tumaini kwa njia ya kuvumilia na kufarijiwa sawa tunavyofundishwa katika Maandiko Matakatifu.
Watu hao walikuwa wenye nia nzuri zaidi kuliko watu wa Tesalonika; nao walipokea Neno la Mungu kwa hamu kubwa. Kila siku walichunguza Maandiko Matakatifu wapate kujua kwamba maneno Paulo aliyosema yalikuwa ya haki.
Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Wafu wako wataishi tena, miili yao itafufuka. Wanaolala katika mavumbi wataamuka na kuimba kwa furaha! Mungu atapeleka umande wake wa uzima, nao wanaokuwa kwa wafu watatoka wazima.