Halafu Yesu akalaani muti ule, akisema: “Tangia sasa hata milele, mutu asipate tena tunda tokea juu yako.” Nao wanafunzi wake wakasikia maneno hayo aliyosema.
Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota, hata mbele hawajatoa mizizi kama miti katika udongo, Yawe akiwapulizia wananyauka, upepo mukali unawapeperusha kama makapi!
Kufika kwao kunaleta machafuko katika karamu zenu za upendo. Wanakula na kushiba pamoja nanyi pasipo haya yoyote. Wao ni kama mawingu yanayopeperushwa na upepo pasipo kuleta mvua. Wao ni kama miti isiyozaa matunda hata wakati wa mavuno; ni miti iliyoongolewa na kufa kabisa.