Nasi vilevile tunazungukwa na kundi kubwa kama lile la wale walioshuhudia imani yao. Basi tutupilie mbali vitu vyote vinavyotusonga, nazo zambi zinazotufunga upesi na tukimbie kwa juhudi sana katika mashindano tunayowekewa.
Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya, akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu wa tumbo, Simoni (aliyeitwa Petro) na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa.