Yesu alipoendelea mbele kidogo, akawaona wandugu wengine wawili: Yakobo na Yoane waliokuwa wana wa Zebedayo. Walikuwa ndani ya chombo wakitengeneza nyavu zao.
Yesu alipoendelea mbele kidogo, akawaona wandugu wengine wawili, Yakobo na Yoane, waliokuwa wana wa Zebedayo. Walikuwa ndani ya chombo pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita.
Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya, akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu wa tumbo, Simoni (aliyeitwa Petro) na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa.
Wakati Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu za tumbo: Simoni na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa lile.
Yesu akaingia ndani ya moja kati ya vile vyombo, nacho kilikuwa cha Simoni. Yesu akamwomba akisukume mbali kidogo na kivuko. Halafu akaikaa mule na kuwafundisha watu.