Luka 5:10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
10 Yakobo na Yoane wana wa Zebedayo waliokuwa wavuvi wenzake na Simoni, walishangaa vilevile. Na Yesu akamwambia Simoni: “Usiogope; tangia sasa utafanya kazi ya kuopoa watu.”
Halafu wakawafanyia wale wenzao waliokuwa ndani ya chombo kingine alama kwa mikono, kusudi wakuje kuwasaidia. Wakakuja, wakajaza vyombo vyote viwili na samaki wengi, hata vyombo vikaanza kuzama.
Kwa ngambo ya Tito, yeye ni mwenzangu, ninafanya kazi pamoja naye kwa ajili yenu. Nao wale wandugu wengine wanaomusindikiza, ni wajumbe wa makanisa wanaotumika kwa ajili ya utukufu wa Kristo.
Yesu alipoendelea mbele kidogo, akawaona wandugu wengine wawili, Yakobo na Yoane, waliokuwa wana wa Zebedayo. Walikuwa ndani ya chombo pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita.
Simoni Petro, Toma (anayeitwa Pacha), Natanaeli (wa muji Kana katika Galilaya), nao wana wa Zebedayo pamoja na wanafunzi wengine wawili wa Yesu, wote walikuwa pamoja.