Siku Bwana atakaporudi, itatimia kama vile mwizi anavyokuja. Siku ile mbingu zitatoweka kwa shindo kubwa, na viumbe vyote vinavyoangaza katika mbingu vitayeyuka. Dunia na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake vitateketezwa.
Basi ukumbuke mafundisho uliyopokea na yale uliyosikia. Uyashike na kugeuka toka zambi zako. Kama usipokesha, nitakuja kama mwizi, wala hautajua saa nitakapokuja kwako.
“Sikiliza, ninakuja kwa saa isiyozaniwa kama vile mwizi. Heri yule anayekesha na kutunza nguo zake vizuri kusudi asitembee uchi na kujifezehesha mbele ya watu.”