Ee Yawe, wewe unatafuta uaminifu siku zote. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa maonyo. Wamevifanya vichwa vyao kuwa vigumu kuliko jiwe; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Wewe umejichokesha bure na washauri wako. Basi, wajitokeze hao wenye akili wakuokoe! Wao wanagawanya mbingu sehemusehemu, wanachunguza nyota na kutabiri kila mwezi yatakayokupata.