Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Isaya 15:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

4 Watu wa Hesiboni na Eleale wanalia, sauti zao zinasikilika mpaka Yasa. Hata waaskari wa Moabu wanalia kwa sauti; mioyo yao inatetemeka.

Gade chapit la Kopi




Isaya 15:4
19 Referans Kwoze  

Kilio cha watu wa Hesiboni kinasikilika huko Eleale mpaka Yasa; kinaenea kutoka Soari mpaka Horonaimu na kufika hata Eglati-Selisia. Hata maji ya kijito Nimurimu yamekauka.


Na kwa muda ule, watu watatafuta kifo, lakini hakitawapata. Watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.


Jua lilipotokea, Mungu akaleta upepo mukali kutoka upande wa jangwa, jua likamuchoma sana Yona juu ya kichwa, karibu azimie. Akatamani kufa, akisema: Ni vizuri kwangu kufa kuliko kuishi.


Basi, sasa ee Yawe, ninakusihi uniondoe uzima wangu, maana ni vizuri kwangu kufa kuliko kuishi.


Kwa nini nilitoka katika tumbo la mama yangu? Nilitoka kusudi nipate taabu na huzuni na kuishi maisha ya haya?


Watu wote watakaobaki wa jamaa hii mbaya, pahali popote pale nilipowasambaza, wataona heri kufa kuliko kuishi. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.


naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia katika jangwa. Basi, akafika, akaikaa chini ya muti mumoja wa muretemu. Halafu, akaomba apate kufa, akisema: “Inatosha! Siwezi tena. Ee Yawe, sasa utoe uzima wangu. Mimi si bora kuliko babu zangu.”


Lakini Sihoni hakuwakubali Waisraeli wapite katika inchi yake. Basi, Sihoni akakusanya watu wake wote, akapiga kambi kule Yahasa, akawashambulia Waisraeli.


Yasa, Kedemoti, Mefati,


Kisha Sihoni akatoka na watu wake wote kupigana nasi karibu na muji wa Yahasa.


Lakini Sihoni hakuwaruhusu Waisraeli wapite katika inchi yake. Akawakusanya watu wake, akaenda Yahasa katika jangwa kwa kuwashambulia Waisraeli.


Ikiwa hivi ndivyo utakavyonitendea, afazali uniue mara moja! Kama ninapata kukubaliwa mbele yako, usiniache kuendelea katika taabu yangu.


Rebeka akamwambia Isaka: “Sina raha kabisa katika maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti wa Esau. Ikiwa Yakobo ataoa mumoja wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”


Maana moto ulitoka Hesiboni, miali ya moto ilitoka katika muji kwa Sihoni, ukauteketeza muji wa Ari wa Moabu, ukaiangamiza milima ya muto Arnoni.


Hukumu imeifikia miji ya nafasi ya uwanja: Holoni, Yahasa, Mefati,


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite