Wakasema: ‘Watumishi hawa wa mwisho wametumika kazi kwa saa moja tu, nawe umewalipa sawasawa na sisi tuliovumilia muchoko na jua kali kwa muchana kutwa!’
Halafu Balamu akamwambia Balaki: Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa kwa moto, nami niende. Labda Yawe atakutana nami. Chochote atakachonionyesha nitakuja kukuambia. Basi, Balamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mulima.