25 Halafu Balaki akamwambia Balamu: Basi, usiwalaani wala usiwabariki kabisa!
Angalia! Waisraeli wameinuka kama simba dike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize windo lake, na kunywa damu ya windo.
Lakini Balamu akamujibu Balaki: Sikukuambia kwamba kile Yawe anachosema ndicho ninachopaswa kufanya?