Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Ezra 9:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

3 Nilipoyasikia maelezo hayo, nikapasua nguo zangu na koti langu, nikaongoa nywele zangu na ndevu zangu kwa huzuni kubwa na kuikaa chini na kufazaika.

Gade chapit la Kopi




Ezra 9:3
21 Referans Kwoze  

Niliposikia hayo nikaikaa chini na kulia, nikaomboleza kwa siku za kutosha. Nikafunga kula na kumwomba Mungu wa mbinguni,


Yoshua akapasua nguo yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini ya Sanduku la Yawe mpaka magaribi; wakajitia mavumbi juu ya vichwa vyao.


Enyi watu wa Yuda, munyoe vichwa vyenu kwa kuwaomboleza watoto wenu wapenzi; mupanue upaa wenu ukuwe mupana kama wa tai, maana watoto wenu watawaacha kwenda katika uhamisho.


Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shuguli za mufalme. Lakini yale maono yalishangaza, nami sikuweza kuyaelewa.


basi, ni wewe, ee mufalme, ambaye umekuwa mukubwa na mwenye nguvu. Ukubwa wako umefika mpaka mbinguni, na ufalme wako umeenea mpaka miisho ya dunia.


Watavaa gunia, hofu itawashika, nao watapata haya na vichwa vyao vyote vitanyolewa.


Nikawafikia wale watu waliokuwa katika uhamisho, waliokuwa wakiishi karibu na muto Kebari huko Teli-Abibu. Nikakaa nao kwa muda wa siku saba nikishangaa sana.


Lakini, ingawa mufalme na watumishi wake wote waliyasikia maneno hayo yote, hawakuogopa wala kurarua nguo zao kwa huzuni.


Munyoe nywele zenu na kuzitupa, enyi wakaaji wa Yerusalema: mufanye maombolezo juu ya vichwa vya milima, maana, mimi Yawe nimewakataa ninyi, nimewatupilia ninyi kizazi kilichosababisha hasira yangu!


Watu wa Diboni wamepanda katika hekalu pahali pa juu kwa kuomboleza, watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba; vichwa vyote vimenyolewa upaa, ndevu zao zote zimekatwa kabisa.


Roho yangu imeregea kabisa; moyo wangu unaugua.


Mumwambie Mungu: “Matendo yako ni ya ajabu! Kwa nguvu yako kubwa waadui zako wanaishiwa nguvu.


Kisha Yobu akasimama, akapasua nguo yake, akanyoa nywele zake, akajitupa chini na kumwabudu Mungu,


Nikawakaripia na kuwalaani, hata nikawapiga wamoja kati yao na kuwaongoa nywele zao. Nikawalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema: “Wabinti zenu musiwaoeshe kwa vijana wao, wala wabinti zao wasiolewe na vijana wenu au na ninyi wenyewe.


Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa musimamizi wa nyumba ya kifalme, Sebuna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi, wakamwendea Hezekia wakiwa na nguo zenye kupasuliwa, wakamwelezea maneno ya yule jemadari.


Wazao wa Haruni wasijinyoe upaa kwa kuomboleza wala wasikate pembe za ndevu zao wala kujichanja chanjo juu ya mwili.


Daudi akapasua nguo yake kwa huzuni. Hata watu waliokuwa pamoja na Daudi wakafanya vilevile.


Ninashikwa na hasira kali, ninapoona waovu wakivunja sheria yako.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite