Pahali pale kulikuwa kumepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya samawi. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za feza kwa kamba za kitani safi nyekundu-nyeusi, na kutundikwa kwenye nguzo za mawe ya marimari. Viti vya zahabu na feza vilikuwa vimewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi ya marimari, nyekundu, nyeusi, manjano na nyeusi.