2 Wakorinto 1:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
4 Yeye anatufariji katika taabu yetu yote, kusudi tupate kuwafariji wale wanaokuwa katika taabu yoyote kwa kuwaletea faraja tuliyopokea kutoka kwa Mungu.
Hii ndiyo maana tumefarijiwa. Lakini zaidi ya kufarijiwa kwetu tulifurahi tena sana kwa ajili ya furaha Tito aliyokuwa nayo kufuatana na jinsi mulivyomutuliza.
Mimi Yawe nitaufariji Sayuni, nitatengeneza pahali pake pote palipoharibika. Nitazifanya mbuga zake kama shamba la Edeni, jangwa yake kama bustani ya Yawe. Ndani yake kutapatikana furaha na shangwe, na nyimbo za shukrani zitasikilika humo.
Hawatasikia tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wenye kuunguza wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemichemi za maji.