Walimu hawa wa uongo ni kama nyama wasiokuwa na akili ambao wanazaliwa tu kwa kunaswa na kuchinjwa. Wao wanasema vibaya juu ya mambo yote wasiyojua. Wataangamizwa kufuatana na ubaya wao wenyewe.
yeye anajaa majivuno wala hajui kitu. Yeye yuko na ulema wa kubishana na kugombezana juu ya maana ya maneno. Na hayo yanaleta wivu, makelele, matukano, masingiziano
Watu wamoja walishuka toka Yudea kwenda Antiokia, nao wakaanza kuwafundisha wandugu waamini kwamba hawawezi kuokoka ikiwa hawatahiriwi sawa vile inavyoagizwa katika Sheria ya Musa.