Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




1 Samweli 4:21 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

21 Naye akamwita mutoto wake Ikabodi, maana alisema: “Utukufu wa Mungu umeondolewa kwa Waisraeli”, akiwa na maana kwamba Sanduku la Agano lilikuwa limetekwa, tena baba mukwe wake na mume wake, wote walikufa.

Gade chapit la Kopi




1 Samweli 4:21
12 Referans Kwoze  

Ee Yawe, ninapenda makao yako, pahali utukufu wako unapokaa.


Aliacha kitambulisho cha nguvu yake kinyanganywe, utukufu wake utiwe katika mikono ya waadui.


Kuna taifa ambalo limekwisha kubadilisha miungu yao ingawa miungu hiyo si miungu? Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyokuwa na faida yoyote.


Makuhani wao walikufa kwa upanga, wala wajane wao hawakuomboleza.


Hata kama wakilea watoto, sitamwacha hata mumoja wao muzima. Ole kwao, nitakapowaacha peke yao!


Sanduku la Agano la Mungu lilitekwa, na wale wana wawili wa Eli, Hofuni na Finehasi, wakauawa.


walibadilisha utukufu wa Mungu kwa sanamu ya nyama ambaye anakula majani.


Akasema: “Utukufu wa Mungu umeondolewa kwa Waisraeli maana Sanduku la Agano la Yawe limetekwa.”


Ahiya mwana wa Ahitubu ndugu yake na Ikabodi mwana wa Finehasi mujukuu wa Eli kuhani wa Yawe katika muji wa Shilo, alikuwa ndiye aliyevaa kizibao cha kuhani. Watu hawakujua kwamba Yonatani amekwisha ondoka.


Na litakalowapata watoto wako wawili, Hofuni na Finehasi, ni hili: Wote wawili watakufa siku moja. Hiki kitakuwa ni kitambulisho kwako.


Siku hiyo, nitatimiza yale yote niliyosema tangu mwanzo mpaka mwisho juu ya Eli na juu ya jamaa yake.


Kwa hasira yake, Yawe amewaweka watu wa Sayuni katika giza. Ametupa toka mbinguni mpaka katika dunia utukufu wa Israeli. Kwa siku ya hasira yake, alilitupilia mbali hata hekalu lake.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite