Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




1 Samweli 30:8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

8 Daudi akamwomba Yawe shauri: “Nikifuata kundi hili nitalikamata?” Yawe akamujibu: “Ulifuate maana utalipata na kuwaokoa hao waliotekwa.”

Gade chapit la Kopi




1 Samweli 30:8
21 Referans Kwoze  

Daudi aliokoa kila kitu Waamaleki walichokuwa wameteka, hata na wake zake wawili.


Basi, Daudi akamwomba Yawe shauri: “Niende kuwashambulia Wafilistini hawa?” Yawe akamujibu: “Ndiyo, kwenda kuwashambulia Wafilistini na kuuokoa muji wa Keila.”


Basi, Daudi alimwuliza Yawe shauri: “Niende kuwashambulia Wafilistini? Utawatia katika mikono yangu?” Naye Yawe akamwambia Daudi: “Kwenda, maana hakika nitawatia Wafilistini katika mikono yako.”


Daudi alipomwomba Yawe shauri, Yawe alimwambia: “Usiwashambulie kutoka hapa unapokuwa, lakini zunguka nyuma yao na kuwashambulia kutokea mbele ya miti ya miforosadi.


Daudi akamwomba tena Yawe shauri, naye Yawe akamwambia: “Simama uende Keila maana nitawatia Wafilistini katika mikono yako.”


Basi Waisraeli wakaenda juu, wakamulilia Yawe mpaka magaribi. Kisha wakaomba shauri kwa Yawe: “Twende tena kupigana na wandugu zetu, wa kabila la Benjamina?” Yawe akawajibu: “Muende mupigane nao.”


Akiniita, mimi nitamwitikia; akikuwa katika taabu nitakuwa pamoja naye, nitamwokoa na kumupa heshima.


Uniite wakati wa taabu, nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”


Yeye atamutegemea kuhani Eleazari ambaye atamujulisha mapenzi yangu kwa kutumia jiwe la shauri. Kwa njia hii, Eleazari atamwongoza Yoshua na Waisraeli wote wanapotoka na wanapoingia.


Hata alipomwomba Yawe shauri, Yawe hakumujibu kwa ndoto, kwa mawe ya kupiga kura, wala kwa njia ya manabii.


Waisraeli wakaenda Beteli kuomba shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benjamina. Yawe akataja kabila la Yuda liende kwanza.


Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa Haruni alikuwa na kazi ya kutumika mbele yake. Waisraeli wakamwuliza Yawe: “Twende tena kupigana na wandugu zetu, watu wa kabila la Benjamina?” Yawe akawaambia: “Muende. Kesho nitawatia katika mikono yenu.”


Hivyo, Saulo akamwuliza Mungu: “Niende kuwashambulia Wafilistini? Utawatia katika mikono ya Waisraeli?” Lakini Mungu hakujibu kitu siku hiyo.


Basi, Abramu akakomboa mali yote iliyonyanganywa na waadui, na kumukomboa mwipwa wake Loti, mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine.


Adui akajisemesha: ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya vitu mpaka hamu yangu iishe. Tutafuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mukono wetu.’


Chochote kilichokuwa chao, kikuwe kikubwa au kidogo, mutoto mwanaume au mwanamuke, Daudi alikikomboa.


Gideoni na wenzake mia tatu wakafika Yordani, wakavuka. Ingawa walikuwa wamechoka sana, waliendelea kuwafuatilia waadui zao.


Wakamwuliza Mungu tena: “Kuna mutu zaidi anayekuja?” Yawe akawajibu: “Anajificha kwenye mizigo.”


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite