Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




1 Samweli 14:41 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

41 Saulo akasema: “Ee Yawe wa Israeli, kwa nini haujanijibu mimi mutumishi wako? Ee Yawe wa Israeli, ikiwa kosa liko kwangu au kwa Yonatani mwana wangu, basi, jiwe la Urimu lionekane. Lakini ikiwa kosa hilo liko kwa watu wako Waisraeli, jiwe la Tumimu lionekane.” Yonatani na Saulo walipatikana kuwa na kosa, lakini watu walionekana hawana kosa.

Gade chapit la Kopi




1 Samweli 14:41
9 Referans Kwoze  

Kisha wakaomba wakisema: “Bwana, wewe unayejua yanayokuwa ndani ya mioyo ya watu wote, utuonyeshe ni nani uliyemuchagua kati ya hawa wawili


Kisha wale watumishi wa mashua wakasemezana: Tupige kura tupate kujua hasara hii imetupata kwa ajili ya kosa la nani. Basi, wakapiga kura; kura ikamwangukia Yona.


Kura inapigwa kwa kujua yatakayotukia, lakini uamuzi ni wa Yawe.


Halafu wakapiga kura, na kura ikamwangukia Matia. Naye akaongezwa katika kundi la wale mitume kumi na mumoja.


Kwa hiyo, Saulo akawaambia: “Ninyi wote musimame upande ule, halafu mimi na mwana wangu Yonatani tutasimama upande huu.” Wao wakajibu: “Fanya chochote unachoona kinafaa.”


Saulo akasema: “Mupige kura kati yangu na mwana wangu Yonatani.” Yonatani akapatikana kuwa na kosa.


Kura inakomesha ubishi; inaamua kati ya wakubwa wanaopingana.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite