Wayuda waliokaa kati ya waadui zetu waliposikia maneno yao, mara kwa mara, walitufikia mara kumi wakisema: “Watakuja toka kila pahali wanapokaa na kutushambulia.”
Lakini wewe, ee Yawe, unajua mashauri yao ya kuniua. Usiwasamehe uovu wao, wala kufuta zambi zao. Waanguke chini mbele yako; uwapige wakati wa hasira yako.
Uwaazibu kwa ajili ya uovu wao wote. Uwatendee kama ulivyonitendea mimi, kwa sababu ya makosa yangu yote. Ninaugua sana kwa maumivu na moyo wangu unazimia.