Sehemu inayofuata, inayoelekeana na nyumba yake ikajengwa upya na Yedaya mwana wa Harumafu. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Hatusi mwana wa Hasabunia.
Benjamina na Hasubu wakajenga upya sehemu inayoelekeana na nyumba yao. Azaria mwana wa Masea, mujukuu wa Anania, akajenga upya sehemu inayoelekeana na nyumba yao.
Zadoki mwana wa Imeri akajenga upya sehemu inayoelekeana na nyumba yake. Sehemu inayofuata, ikajengwa upya na Semaya mwana wa Sekania, mulinzi wa Mulango wa Mashariki,
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya mulango wa Farasi kuelekea upande wa mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Yawe. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.