Nehemia 3:10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
10 Sehemu inayofuata, inayoelekeana na nyumba yake ikajengwa upya na Yedaya mwana wa Harumafu. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Hatusi mwana wa Hasabunia.
Benjamina na Hasubu wakajenga upya sehemu inayoelekeana na nyumba yao. Azaria mwana wa Masea, mujukuu wa Anania, akajenga upya sehemu inayoelekeana na nyumba yao.
Walawi, ni kusema Yesua, Kadimieli, Bani, Hasabuea, Serebia, Hodia, Sebania na Petahia, wakawaambia watu: Musimame na kumusifu Yawe, Mungu wenu. Mumusifu milele na milele! Na watu wakasifu jina lako tukufu, ambalo linatukuka kuliko baraka na sifa zote.