Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -




Nehemia 12:8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

8 Walawi walikuwa: Yesua, Binui, Kadimieli, Serebia, Yuda na Matania, ambaye alishugulika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake.

Faic an caibideil Dèan lethbhreac




Nehemia 12:8
12 Iomraidhean Croise  

Jamaa zingine za Walawi zilisimamia kazi ya nyimbo katika hekalu. Waliishi katika vyumba vimoja vya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi ingine yoyote kwa maana walikuwa wakitumika usiku na muchana.


Walawi wa ukoo wa Yesua na wa Kadimieli, wazao wa Hodavia waliorudi kutoka katika uhamisho walikuwa makumi saba na wane.


Yesua mwana wa Yosadaki, pamoja na makuhani wenzake, na Zerubabeli, mwana wa Sealtieli, pamoja na wandugu zake, wakaijenga upya mazabahu ya Mungu wa Israeli, kusudi waweze kumutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, mutu wa Mungu.


na Matania mwana wa Mika mwana wa Zabudi, wa uzao wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba maombi ya shukrani. Bakubukia alikuwa musaidizi wake. Pamoja nao kulikuwa Abuda mwana wa Samua mwana wa Galali wa uzao wa Yedutuni.


Kiongozi wa Walawi waliokaa Yerusalema alikuwa, Uzi, mwana wa Bani mwana wa Hasabia mwana wa Matania mwana wa Mika wa ukoo wa Asafu, waliokuwa waimbaji, viongozi waangalizi wa shuguli za nyumba ya Mungu.


Viongozi wa Walawi Hasabia, Serebia, Yesua mwana wa Kadimieli walisimama kuelekeana na wandugu zao walipangwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na kushukuru, kufuatana na amri ya mufalme Daudi, mutu wa Mungu.


Nao Bakubukia na Uno warafiki zao, walisimama wakielekeana nao katika ibada.


Walawi wa ukoo wa Yesua, ni kusema Kadimieli, wazao wa Hodavia waliorudi kutoka katika uhamisho walikuwa makumi saba na wane.


Kuliwekwa daraja la Walawi; pale kulisimama Yesua, Bani, Kadimieli, Sebania, Buni, Serebia, Bani na Kenani. Wakamwomba kwa sauti kubwa Yawe, Mungu wao.


Lean sinn:

Sanasan


Sanasan