Yawe anasema: Watu wangu ni wapumbafu, hawanijui mimi. Wao ni watoto wajinga; hawana ufahamu. Wao wanaelewa vizuri kutenda maovu, lakini hawajui kutenda mema.
Kwa maana zamani sisi vilevile tulikuwa wajinga, waasi na wapotovu. Tulikuwa tumetawaliwa na kila namna ya tamaa mbaya na ya vitu mbalimbali vilivyotuvuta sana. Tuliishi katika uovu na wivu, tuliwachukiza watu nao walituchukia.