Kama vile mwanadamu alivyokuja katika dunia akiwa uchi toka katika tumbo la mama yake, ndivyo atakavyorudi uchi kule alikotoka. Hataweza kupeleka hata sehemu ndogo ya mapato ya kazi yake.
Watu wa Efuraimu wanachunga upepo, muchana kutwa wanafukuza upepo wa mashariki. Wanazidisha uongo na mateso, wanafanya mapatano na Asuria na kupeleka mafuta Misri.