Kwa maana, tunajua kwamba hema hii tunayoishi ndani yake hapa katika dunia, maana yake mwili wetu, itakapobomolewa, Mungu atatupatia makao mengine mbinguni. Nayo ni nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na inayodumu milele.
Yawe, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mutaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mukishika amri zake ambazo ninawapa leo na kuwa waangalifu kwa kuzitimiza,