Kisha nikaona mateso yote yanayofanyika chini ya jua. Watu wanaogandamizwa wanalia machozi, lakini hakuna mutu yeyote anayewafariji. Wagandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.
Usishangae ukiona katika inchi wamasikini wanagandamizwa, wananyimwa haki na sheria zao. Kila mwenye cheo anayewatesa wamasikini yupo chini ya mukubwa mwingine, na juu ya hao wote kuna wakubwa zaidi.
Wote ni wafundi wa kutenda maovu; waongozi na waamuzi wanaomba kituliro. Wakubwa wanaonyesha wazi nia zao mbaya, nao wanashirikiana pamoja kwa kuzitimiza.
Halafu Paulo akamwambia: “Mungu yeye mwenyewe atakupiga kofi, wewe unayeonekana kwa inje kama ukuta uliopakaliwa chokaa! Wewe unaikaa pale kwa kunihukumu kufuatana na Sheria. Lakini wewe mwenyewe unaivunja kwa kuamuru wanipige!”