18 Maana katika kuwa na hekima nyingi kuna wasiwasi; na anayeongeza maarifa zaidi anaongeza huzuni zaidi.
Kisha Mungu akamwambia mwanadamu: Sikia! Kumwogopa Bwana ndiyo hekima, na kujitenga na uovu ndiyo maarifa.
Basi, nikasema ndani ya moyo wangu: “Yatakayomupata mupumbafu yatanipata na mimi vilevile. Kwa nini, basi, nimekuwa na hekima zaidi?” Nikasema ndani ya moyo wangu: “Hayo nayo ni bure.”
Maisha yake yote yamejaa taabu, na jasho yake ni mahangaiko matupu. Hata usiku akili yake haipumziki! Hayo nayo ni bure.
Basi, usikuwe wa haki kupita kipimo, wala usikuwe mwenye hekima zaidi! Kwa nini kujiangamiza wewe mwenyewe?