18 Kama alikukosea au kama yuko na deni yako ya kitu chochote, unidai mimi.
Mimi mwenyewe nitakuwa rehani kwake. Wewe utanidai mimi. Nisipomurudisha umwone kwa macho yako mwenyewe, kosa likuwe juu yangu milele.
Basi kama unaendelea kunihesabu kuwa mwenzako, umupokee kama vile ungenipokea mimi mwenyewe.
Mimi Paulo ninaandika kwa mukono wangu mwenyewe maneno haya: nitakulipa. (Sitaki kusema kwamba maisha yako ni deni unalokuwa nalo kwangu.)