Danieli 7:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20029 Nilipokuwa nikiendelea kuangalia, nikaona viti vya kifalme viliwekwa hapo, kisha Muzee mumoja wa zamani sana akakuja, akaikaa. Alikuwa amevaa nguo nyeupe kama teluji; nywele zake zilikuwa kama sufu safi. Kiti chake cha kifalme kilikuwa ndimi za moto, na magurudumu ya kiti kile yalikuwa moto unaowaka. Faic an caibideil |
Kisha nikaona viti vya kifalme na watu waliokuwa wakiikaa juu yao, wakapewa uwezo wa kuhukumu. Nikaona vilevile roho za wale waliochinjwa kwa sababu ya kutangaza ukweli ulioshuhudiwa na Yesu na Neno la Mungu. Watu wale hawakumwabudu yule nyama wa ajabu, wala sanamu yake, wala hawakupigwa chapa yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Nao wakafufuka na kutawala pamoja na Kristo muda wa miaka elfu moja.