Danieli 7:7 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20027 Kisha, katika maono hayo yangu ya usiku, nikaona nyama wa ine wa ajabu na wa kutisha, mwenye nguvu sana. Huyu alikuwa na meno makubwa ya chuma ambayo aliyatumia kwa kula na kuvunjavunja, na mabaki aliyakanyagakanyaga. Alikuwa tofauti na wale nyama wengine watatu, maana alikuwa na pembe kumi. Faic an caibideil |
Yule nyama uliyemwona alikuwa yuko zamani, lakini sasa hayuko tena. Naye ni tayari kupanda toka katika shimo la kuzimu na kwenda kuangamizwa kabisa. Nao wakaaji wa dunia ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uzima tangia kuumbwa kwa dunia, watashangaa wakati watakapomwona yule nyama, kwa sababu alikuwa yuko zamani lakini hayuko sasa, naye atatokea tena!