Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

ZAKARIA 10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Mungu anaahidi ukombozi

1 Muombe Yawe awape mvua za masika. Yawe ndiye anayeleta mawingu ya mvua; ndiye anayewapa watu mvua za manyunyu, na kustawisha mimea katika shamba kwa ajili ya wote.

2 Sanamu zao za kupigia ramuli ni uongo mutupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto danganyifu, na kuwapa watu faraja za bure. Ndiyo maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika maana wamekosa muchungaji.

3 Yawe anasema hivi: Nimewaka hasira juu ya hao wachungaji, nami nitawaazibu hao watawala. Mimi Yawe wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.

4 Kwa ukoo wa Yuda kutatokea: watawala wa kila namna, wakubwa wenye nguvu kama jiwe kubwa la musingi, wanaokuwa imara kama musumari wa hema, wenye nguvu kama upinde wa vita.

5 Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa katika vita, watawakanyaga waadui zao ndani ya matope katika njia. Watapigana kwa sababu mimi Yawe nipo pamoja nao; nao watawafezehesha hata waaskari wapanda-farasi.

6 Nitawaimarisha watu wa Yuda; nitawaokoa wazao wa Yosefu. Nitawarudisha kwao kwa maana ninawaonea huruma, nao watakuwa kama vile sikuwa nimewakataa. Mimi ni Yawe, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.

7 Watu wa Efuraimu watakuwa kama mashujaa katika vita; watajaa furaha kama watu waliokunywa divai. Watoto wao wataona hayo na kufurahi, watajaa furaha ndani ya moyo kwa sababu yangu mimi Yawe.

8 Nitawaita watu wangu na kuwakusanya pamoja; nimekusudia kuwakomboa, nao watakuwa wengi kama vile mbele.

9 Japo niliwatawanya kati ya mataifa, hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo. Nao pamoja na watoto wao wataishi na kurudi katika nyumba zao.

10 Nitawarudisha kutoka inchi ya Misri, nitawakusanya kutoka Asuria; nitawaleta katika inchi ya Gileadi na Lebanoni, nao watajaa kila nafasi katika inchi.

11 Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya muto Nili vitakauka. Kiburi cha Asuria kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka.

12 Mimi nitawaimarisha watu wangu, nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza. Ni mimi Yawe ninayesema hivyo.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan