Zaburi 93 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Mungu mufalme 1 Yawe anatawala; amejifunika utukufu mukubwa! Yawe amevaa utukufu na nguvu! Ameimarisha ulimwengu, hautatikisika hata kidogo. 2 Kiti chako cha kifalme ni imara tangu zamani; wewe umekuwa mbele ya nyakati zote. 3 Ee Yawe, bahari zimetoa sauti; zimenyanyua sauti zao, bahari zinanyanyua tena uvumi wao. 4 Yawe ana mamlaka juu mbinguni, ana nguvu kuliko mulio wa bahari, ana nguvu kuliko mawimbi ya maji. 5 Ee Yawe, maagizo yako ni imara; nyumba yako ni takatifu milele. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo