Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 88 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Kilio cha musaada

1 Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Wakora: Kwa mutindo wa wimbo wa huzuni. Mashairi ya Hemani Mwezra.

2 Ee Yawe, mwokozi wangu, ninalia muchana kutwa, na usiku ninakulalamikia.

3 Maombi yangu yakufikie, usikilize kilio changu.

4 Hasara inanipita kipimo, nami niko karibu kufa.

5 Ninaonekana kama mutu anayeshuka katika shimo la wafu. Nguvu zangu zote zimeniishia.

6 Ninahesabiwa kati ya wafu, kama waliouawa, wanaokuwa katika kaburi, kama wale ambao hauwakumbuki tena, ambao wametengwa na ulinzi wako.

7 Umenitupa mbali katika shimo la wafu, katika giza kubwa.

8 Hasira yako imenilemea; umenisonga kwa zoruba yako yote.

9 Umewafanya warafiki zangu waniepuke, umenifanya kuwa chukizo kwao. Nimefungwa wala siwezi kutoroka.

10 Macho yangu yamefifia kwa huzuni. Kila siku ninakulilia, ee Yawe. Ninakunyooshea mikono yangu.

11 Wewe unawatendea wafu maajabu yako? Waliokufa wanafufuka na kukusifu?

12 Wema wako unatajwa ndani ya kaburi, au uaminifu wako katika shimo la kuangamia?

13 Maajabu yako yanajulikana humo katika giza, au matendo yako ya haki katika inchi ya waliosahauliwa?

14 Mimi ninakulilia, ee Yawe. Kila asubui ninakuletea ombi langu.

15 Mbona, ee Yawe, unanitupilia mbali? Kwa nini unanificha uso wako?

16 Nimeteseka na kukaribia kifo tangu ujana wangu; ninateseka kwa mapigo yako, niko tabani kabisa.

17 Kasirani yako imeniwakia; mashambulio yako ya kutisha yananiangamiza.

18 Yananizunguka kama mafuriko muchana kutwa; yananizunguka yote pamoja.

19 Umewafanya warafiki na wenzangu wote waniepuke; giza ndilo limekuwa mwenzangu.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan