Zaburi 67 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Wimbo wa shukrani 1 Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa vyombo vyenye nyuzi. Zaburi. Wimbo. 2 Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki, utuelekezee uso wako kwa wema, 3 dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa. 4 Watu wakusifu, ee Mungu, watu wote wakusifu! 5 Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana unawahukumu watu kwa usawa, na kuyaongoza mataifa katika dunia. 6 Watu wakusifu, ee Mungu, watu wote wakusifu! 7 Inchi imetoa mazao yake; Mungu, Mungu wetu, ametubariki. 8 Mungu aendelee kutubariki. Watu wote katika dunia wamwabudu. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo