Zaburi 6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Maombi wakati wa taabu 1 Kutoka Mukubwa wa waimbaji: kwa vyombo vyenye nyuzi nane. Zaburi ya Daudi. 2 Ee Yawe, usiniazibu kwa hasira yako, usiniadibishe kwa kasirani yako. 3 Unihurumie, ee Yawe, nimeishiwa nguvu; uniponyeshe, ee Yawe, ninatetemeka mpaka katika mifupa. 4 Ninahangaika sana ndani ya roho yangu. Ee Yawe, utakawia mpaka wakati gani? 5 Unigeukie, ee Yawe, uniokoe; uniponyeshe kwa sababu ya wema wako. 6 Huko kwa wafu hakuna anayekukumbuka; katika kuzimu ni nani anayeweza kukusifu? 7 Ninatabanika kwa kulia kwa uchungu; usiku ninalowanisha kitanda changu kwa machozi; kwa kulia kwangu ninalowanisha matandiko yangu. 8 Macho yangu yamechoka kwa huzuni; yamefifia kwa kutaabishwa na waadui. 9 Muondoke karibu nami, enyi wote watenda maovu! Maana Yawe amesikia kilio changu. 10 Yawe amesikia ombi langu; Yawe amekubali maombi yangu. 11 Waadui zangu wote watafezeheka na kufazaika; watarudi nyuma na kufezeheka kwa rafla. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo