Zaburi 54 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Maombi ya kujikinga na waadui 1-2 Kwa mukubwa wa waimbaji: kwa vyombo vyenye nyuzi. Mashairi ya Daudi, yanayoelekea wakati mutu mumoja kutoka Zifu alipomwendea Saulo na kumujulisha kwamba Daudi amejificha kwao. 3 Ee Mungu, uniokoe kwa jina lako, unitetee kwa nguvu zako. 4 Ee Mungu, usikilize maombi yangu; uyategee sikio maneno ya kinywa changu. 5 Watu wenye kiburi wananishambulia, watu wakali wanawinda maisha yangu, watu ambao hawamujali Mungu. 6 Ninajua Mungu ni musaada wangu, Yawe anaimarisha maisha yangu. 7 Yeye atawaazibu waadui zangu kwa uovu wao wenyewe; kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize. 8 Nitakutolea sadaka kwa moyo wa furaha; nitalisifu jina lako maana wewe ni muzuri. 9 Umeniokoa katika taabu zangu zote, nami nimewaona waadui zangu wameshindwa. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo