Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 26 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Maombi ya mutu mwema

1 Zaburi ya Daudi. Ee Yawe, unitetee, maana nimeishi katika ukamilifu, nimekutumainia wewe bila kusita.

2 Unijaribu, ee Yawe, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili yangu.

3 Wema wako uko mbele ya macho yangu, ninaishi kutokana na uaminifu wako.

4 Sikusanyiki na watu wapotovu; sishirikiani na watu wanafiki.

5 Ninachukia mikutano ya wabaya; wala sitakusanyika na waovu.

6 Ninanawa mikono yangu kuonyesha kama sina kosa, na kuizunguka mazabahu yako, ee Yawe,

7 nikiimba wimbo wa shukrani, na kueleza matendo yako ya ajabu.

8 Ee Yawe, ninapenda makao yako, pahali utukufu wako unapokaa.

9 Usiniangamize pamoja na wenye zambi, wala usinitupe pamoja na wauaji,

10 watu ambao matendo yao ni maovu kila wakati, watu ambao wanapokea kituliro kila wakati.

11 Lakini mimi ninaishi katika ukamilifu; unihurumie na kunikomboa.

12 Mimi nimesimama pahali penye kuwa imara; nitamusifu Yawe katika kusanyiko kubwa.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan