Zaburi 23 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Mungu ni muchungaji wangu 1 Zaburi ya Daudi. Yawe ni muchungaji wangu; sitapungukiwa na kitu. 2 Ananipumzisha kwenye majani mabichi; ananiongoza kando ya maji matulivu, 3 na kuirudishia nafsi yangu nguvu mupya. Ananiongoza katika njia sawa kwa utukufu wa jina lake. 4 Hata nikipita katika bonde la giza kubwa, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe, ee Yawe, ni pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vinanipa moyo. 5 Umenitayarishia karamu mbele ya waadui zangu. Umekipakaa kichwa changu mafuta. Kikombe changu umekijaza tele. 6 Kweli, uzuri na wema wako vitakuwa pamoja nami siku zote za maisha yangu; nami nitakaa katika nyumba ya Yawe milele. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo