Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 17 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Maombi ya mutu mwema

1 Maombi ya Daudi. Ee Yawe, usikie ombi langu la haki, usikilize kilio changu, uyategee sikio maombi yangu yasiyokuwa ya udanganyifu.

2 Haki yangu ikuje kutoka kwako, maana wewe unajua jambo la haki.

3 Wewe unajua kabisa moyo wangu; umenifikia usiku kunichunguza, umenitia katika majaribu; haukuona uovu ndani yangu, sikusema kitu kisichofaa.

4 Juu ya matendo watu wanayotenda, mimi nimetii amri yako, sikushika njia za watesaji wakali.

5 Nimefuata siku zote njia yako; wala sijatereza hata kidogo.

6 Ee Mungu, ninakuita, maana wewe unanijibu; unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.

7 Onyesha wema wako wa ajabu; uwaokoe kutoka waadui zao wale wanaokimbilia kwako.

8 Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako,

9 mbali na mashambulio ya waovu, mbali na waadui zangu wa hatari wanaonizunguka.

10 Hao hawana huruma yoyote ndani ya moyo; wamejaa maneno ya kujivuna.

11 Wananifuatilia na kunizunguka; wananivizia waniangushe chini.

12 Wako tayari kunirarua kama simba, kama simba mukali anavyovizia nyama.

13 Ee Yawe, simama sasa uwapiganishe na kuwaporomosha! Kwa upanga wako uokoe nafsi yangu kutoka waovu.

14 Ee Yawe, mukono wako uwafukuze kati ya watu, tukio lao likuwe kutengana na wanaokuwa wazima. Uwashibishe kwa akiba uliyowawekea, watoto wao nao washibe na kuacha sehemu, wawaachie hata na wajukuu wao.

15 Lakini mimi nitauona uso wako, maana mimi ni mutu wa haki; nitakapoamuka nitajaa furaha kwa sababu unanitokea.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan