Zaburi 16 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Kuomba usalama 1 Mashairi ya Daudi. Unilinde, ee Mungu, maana ninakimbilia kwako. 2 Ninamwambia Mungu: “Wewe ni Bwana wangu; sina uheri wowote isipokuwa wewe.” 3 Na juu ya waaminifu katika inchi, ninaheshimu nguvu zao. 4 Lakini wanaoabudu miungu mingine, watapata mateso mengi. Sitaitolea sadaka za damu hata kidogo, na majina ya miungu hiyo sitayataja. 5 Wewe, ee Yawe, ndiwe riziki yangu kubwa, majaliwa yangu yako katika mikono yako. 6 Umenipimia sehemu nzuri sana; urizi wangu ni wa kupendeza. 7 Ninamusifu Yawe anayeniongoza. Usiku zamiri yangu inanifundisha. 8 Siku zote Yawe ni mbele yangu; yeye yuko pamoja nami, wala sitatikisika. 9 Kwa hiyo nitafurahi kwa moyo wote na kushangilia, nami nitakaa salama kabisa. 10 Kweli wewe unanikinga na nguvu za kuzimu, haumwachi mutakatifu wako aone kaburi. 11 Unanionyesha njia ya kufikia uzima. Kuwa mbele yako ni kujazwa furaha, kuwa kwa kuume kwako kunapendeza milele. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo