Zaburi 141 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Hatari za tamaa mbaya 1 Kwa mukubwa wa waimbaji: Zaburi ya Daudi. Ninakulilia, ee Yawe, ukuje haraka kunisaidia! Usikilize sauti yangu wakati ninapokuita! 2 Upokee maombi yangu kama ubani; ninapoinua mikono yangu kwako, unikubali kama sadaka ya magaribi. 3 Ee Yawe, ulinde kinywa changu, uweke mulinzi kwenye mulango wa kinywa changu. 4 Unikinge nisielekee kufanya mabaya, nisijishugulishe na matendo maovu, nisijiunge na watu wanaotenda mabaya, wala nisishiriki hata kidogo katika karamu zao. 5 Afazali mutu mwema anipige kwa kunionya; lakini sikubali hata kidogo kusifiwa na wabaya, maana ninaomba siku zote juu ya maovu yao. 6 Wakubwa wao watakapopondwa juu ya mawe, ndipo watatambua kwamba maneno yangu yalikuwa mazuri. 7 Mifupa yao itatawanywa kwenye midomo ya kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! 8 Lakini mimi ninakutegemea, ee Yawe, Mungu wangu; ninakimbilia kwako, usiniache katika hatari. 9 Unikinge na mitego waliyonitegea, uniepushe na wavu wa hao watu waovu. 10 Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe, wakati mimi ninaponyoka. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo