Zaburi 140 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Kuomba ulinzi wa Mungu 1 Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi. 2 Ee Yawe, uniokoe na watu wabaya, unikinge na watesaji wakali. 3 Watu hao wanafikiri mabaya siku zote, wanaamusha ugomvi kila mara. 4 Ndimi zao ni hatari kama za nyoka; ndani ya midomo yao kuna maneno ya sumu kama ya piri. 5 Ee Yawe, unilinde na makucha ya wabaya; unikinge na watesaji wakali ambao wamepanga kuniangusha. 6 Wenye kiburi wamenitegea mitego, wametandika kamba kama wavu, wameficha mitego katika njia wanikamate. 7 Ninamwambia Yawe: “Wewe ni Mungu wangu.” Usikilize, ee Yawe, sauti ya ombi langu. 8 Ee Yawe, Bwana wangu, mukombozi wangu mukubwa, umenikinga salama wakati wa vita. 9 Ee Yawe, usiwape waovu vitu wanavyotaka, wala mipango yao mibaya usiifanikishe. 10 Hao wanaonizunguka wanainua vichwa; uovu wa maneno yao uwapate wao wenyewe! 11 Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe katika mashimo, wasiinuke tena. 12 Wanaosingizia wengine wasifanikiwe katika inchi; uovu uwapate watesaji wakali na kuwaangamiza bila kukawia! 13 Ninajua kwamba Yawe anatetea wamasikini na kuwapatia wakosefu haki. 14 Hakika watu wa haki watasifu jina lako; watu wa usawa watakaa kwako. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo