Zaburi 138 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Maombi ya shukrani 1 Zaburi ya Daudi. Ninakushukuru, ee Yawe, kwa moyo wangu wote, ninaimba sifa zako mbele ya miungu. 2 Ninainama uso mpaka chini kuelekea hekalu lako takatifu. Ninalisifu jina lako, kwa sababu ya wema na uaminifu wako. Umeheshimisha jina lako na neno lako kuliko vitu vyote. 3 Nilipokulilia, wewe ulinijibu; umeniongezea nguvu yangu. 4 Wafalme wote katika dunia watakusifu, ee Yawe, kwa sababu wameyasikia maneno yako. 5 Wataimba sifa za matendo yako, ee Yawe, kwa maana utukufu wako ni mukubwa. 6 Ee Yawe, ingawa wewe uko juu ya wote, unawaangalia wanyenyekevu kwa wema; lakini, unatambua wenye kiburi kwa mbali. 7 Hata nikisongwa na taabu, wewe unanilinda. Unanyoosha mukono wako juu ya waadui zangu wakali, kwa nguvu yako kubwa unaniokoa. 8 Ee Yawe, utatimiza yote uliyoniahidia. Wema wako, ee Yawe, unadumu milele. Usisahau kazi ya mukono wako mwenyewe. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo