Zaburi 136 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Wimbo wa shukrani 1 Mumushukuru Yawe kwa sababu yeye ni muzuri! Wema wake unadumu milele! 2 Mumushukuru Mungu wa miungu. Wema wake unadumu milele. 3 Mumushukuru Bwana wa wabwana. Wema wake unadumu milele. 4 Yeye peke yake anatenda miujiza mikubwa. Wema wake unadumu milele. 5 Aliumba mbingu kwa hekima. Wema wake unadumu milele. 6 Alitengeneza inchi juu ya vilindi vya maji. Wema wake unadumu milele. 7 Aliumba jua, mwezi na nyota. Wema wake unadumu milele. 8 Aliumba jua litawale muchana. Wema wake unadumu milele. 9 Aliumba mwezi na nyota vitawale usiku. Wema wake unadumu milele. 10 Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Misri. Wema wake unadumu milele. 11 Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko. Wema wake unadumu milele. 12 Akawaondoa kwa mukono wake wenye nguvu na mamlaka. Wema wake unadumu milele. 13 Aligawanya bahari Nyekundu katika sehemu mbili. Wema wake unadumu milele. 14 Akawapitisha watu wa Israeli humo. Wema wake unadumu milele. 15 Lakini akazamisha mufalme wa Misri na waaskari wake humo. Wema wake unadumu milele. 16 Aliongoza watu wake katika jangwa. Wema wake unadumu milele. 17 Alipiga wafalme wenye nguvu. Wema wake unadumu milele. 18 Akaua wafalme wenye utukufu. Wema wake unadumu milele. 19 Akamwua Sihoni, mufalme wa Waamori. Wema wake unadumu milele. 20 Akamwua Ogi, mufalme wa Basani. Wema wake unadumu milele. 21 Akakamata inchi zao kuwa urizi wa watu wake. Wema wake unadumu milele. 22 Ni urizi wa Israeli, mutumishi wake. Wema wake unadumu milele. 23 Alitukumbuka wakati wa uzaifu wetu. Wema wake unadumu milele. 24 Akatuokoa kutoka waadui zetu. Wema wake unadumu milele. 25 Anapatia kila kiumbe chenye uzima chakula. Wema wake unadumu milele. 26 Mumushukuru Mungu wa mbinguni. Wema wake unadumu milele! |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo