Zaburi 13 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Kuomba musaada 1 Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi. 2 Mpaka wakati gani, ee Yawe, utaendelea kunisahau? Mpaka wakati gani utanificha uso wako? 3 Mpaka wakati gani nitakuwa na wasiwasi katika roho na sikitiko katika moyo siku hata siku? Mpaka wakati gani waadui zangu watanishinda? 4 Uniangalie na kunijibu, ee Yawe, Mungu wangu. Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo. 5 Usiwaache waadui zangu waseme: “Tumemushinda huyu!” Watesaji wangu wasifurahie kuanguka kwangu. 6 Lakini mimi ninatumainia wema wako, moyo wangu ufurahie wokovu wako. Nitakuimbia wewe, ee Yawe, kwa vyote ulivyonitendea! |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo