Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 129 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Maombi juu ya waadui za Israeli

1 Wimbo wa safari za kidini. Kila mutu katika Israeli aseme: “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu”.

2 Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakunishinda.

3 Walinikata vidonda katika mugongo, kama wanavyolima matuta katika shamba.

4 Lakini Yawe ni mwenye haki; ametutosha katika utumwa wa hao waovu.

5 Wafezeheke na kurudishwa nyuma, wote wale wanaouchukia Sayuni.

6 Wakuwe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo zinanyauka mbele ya kukomaa,

7 anayezikata hajazi kitanga cha mukono, wala anayezikusanya haenezi fungu.

8 Naye anayepita karibu asiwaambie: “Yawe awabariki! Tunawabariki kwa jina la Yawe!”

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan